WANAFUNZI 5 NA MLINZI WAMEKUFA KWA WAPIGWA RISASI

Wanafunzi watano na mlinzi mmoja wamepigwa risasi na kuuawa katika shambulio la asubuhi,katika shule moja ya upili Kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa Sudan Kusini.

Mashahidi wanasema watu watatu waliokuwa na silaha,mmoja wao akiwa mwanafunzi wa zamani walivamia mabweni katika Shule ya Upili ya Lokichogio leo asubuhi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema mshambulizi mkuu alikuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo aliyefukuzwa kwenda shuleni baada kupigana na mwenzake ambapo alikuwa ameagizwa kurudi na wazazi wake lakini hakufanya hivyo.
Walioshuhudia walisema mwanafunzi huyo alirudi shuleni usiku wa manane na wenzake wawili ambapo inadaiwa walimpiga risasi na kumuua mlinzi na kisha kwenda katika mabweni wakimtafuta mwanafunzi waliyepigana naye awali.
Mwanafunzi huyo hakuwa shuleni wakati huo na washambuliaji hao waliwapiga risasi na kuwaua wanafunzi watano na kuwabaka wasichana wawili.
Chama cha msalaba mwekundu kimesema kimewahamisha waliojeruhiwa hadi hospitalini.
Lokochogio iko karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia na wakaazi wengi wa eneo hilo hubeba bunduki na ni wachungaji wanaolinda mifugo wao dhidi ya wizi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA