MAUAJI TENA MKOANI KATAVI,SASA MITHILI YA KIBITI USIKU WA KUAMKIA LEO WASIOJULIKANA WAMEUA TENA MKE NA MME,KATIKA SIKU SABA IDADI YAFIKIA WATU 5 WAKIWEMO WANAOPIGWA KWA RISASI



Na.Issack Gerald-Tanganyika Katavi
Watu wawili mke na Mme wanaofahamika kwa majina ya Adam Charles (41) na Katalina Gabriel (39) wakazi wa Kijiji cha Kasekese Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi kwa kukatwakatwa na vitu vinavyosemekana kuwa vyenye ncha kali na watu wasiojulikana.

Inaelezwa kuwa walivamiwa usiku wa saa 7 kuamkia leo na kukatwakatwa sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za kichwani.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasekese Ramadhani Ibrahimu amethibitisha kutokea kwa mauwaji hayo na jinsi tukio lilivyotokea.
Ibrahim amesema baad aya tukio hilo walitoa msaada wa haraka kuwafikisha hospitali Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya Matibabu ambapo licha ya jitihada zao zote ili kuokoa maisha ya wawili hao imehindikana na hatimaye kupoteza maisha.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo na kutoa Msaada wameeleza kusikitishwa na tukio hilo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda alipotafutwa majira ya saa 10 jioni ili kuelezea hatua ambazo zimechukuliwa na jeshi la polisi kutokana na tukio hilo,kamanda Nyanda alisema hana taarifa kuhusu mauaji hayo.
Kuanzia Oktoba 7 mwaka huu,mpaka sasa matukio yapatayo matatu yametokea na kupelekea mauaji kwa watu 5 wilayani Tanganyika.
Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na tukio lililotokea Oktoba 7 likihusisha mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha myamasi aliyeuawa kwa kupigwa risasi ambapo kwa mjibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyamasi mkazi huyo,alipigwa risasi na vyombo vya kamati ya ulizi na usalama vilivyokuwa vikifanya zoezi la kuwaondoa wavamizi wa hifadhi ya misitu Wilayani Tanganyika.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando alithibitisha mtu huyo kuuwawa akisema kuwa amepigwa risasi katika majibizano kati ya raia na vyombo vya kamati ya ulinzi na usalama ambapo pia inaelezwa watu 7 walijerehiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
 Ripoti za Oktoba 12,2017

Mtu mmoja anayefahamika kwa jila la Suzani Chales (40) mkaazi wa Kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amekufa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.Tukio okt 12,2017

Ripoti ya Oktoba 9,2017-

MTU mmoja amepoteza maisha kwa madai ya kupigwa risasi na askari wa maliasili  na wengine wanne kujeruhiwa katika kitongoji cha Mnyamasi wilayani Tanganyika mkoani Katavi,wakati wa oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi-Tukio Okt 7,2017

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA