RAIS AMEWAJIBU SHIRIKISHO L VYAMA VY AWAFANYAKAZI TUCTA



Rais John Pombe Magufuli amesema serikali ya awamu ya tano imewapandisha vyeo na kurekebisha mishahara ya watumishi 59,967 baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki  hewa kukamilika.

Rais Magufuli amesema hayo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu za miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere,sherehe ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar.  
Rais Magufuli katika hotuba hiyo alitolea mfano uzalendo wa Baba wa Taifa ambaye aliamua kupunguza mshahara wake na kukataa kuongeza mishahara ya watumishi wachache huku walio wengi wakipata shida.

“Ninaposema hivyo simaanishi kuwa mishahara isiongezwe. La hasha. Ninachosema ni kwamba kabla ya kudai nyongeza ya mishahara ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa Serikali, lakini pia tutambue kuwa kuna Watanzania wenzetu wengi tu wanaohitaji kuboreshewa huduma.
"Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki, Serikali imewapandisha vyeo na kuwarekebishia mishahara watumishi 59,967 ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 159.33 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka huu na mishahara mipya itaanza kulipwa kuanzia mwaka huu. Na kwa upande wa Zanzibar kima cha chini cha mshahara kimeongezwa kutoka Shilingi 150,000/- hadi kufikia Shilingi 300,000/-”  Amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wiki iliyopita shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA lilikuwa limesema linatarajia kufanya vikao na serikali kujadili tamko la Rais Magufuli kusema kuwa katika kipindi chake chote cha uongozi watumishi wa umma wasitegemee kupandishiwa madaraja na mishahara suala ambalo juzi lilikanushwa na msemaji wa serikali kuwa hakuna kipengele kinachotamka kuwa Rais alisema hataongeza mishahara wala kupandisha madaraja. 
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka vijana kuendelea kujielimisha katika mambo mbalimbali na kuwataka kutojihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA