RAIS MAGUFULI-MWENYE UTAENDELEA NA MBIO ZAKE KAMA KAWAIDA NIKIWA MADARAKANI



Na.Issack Gerald-Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli amesema katika kipindi chake cha uongozi,Mwenge wa Uhuru utaendelea kukimbizwa nchi nzima kila mwaka.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo mashinikzo kutoka kwa watu mbalimbali nchini wakitaka mwenge wa uhuru ufutwe kwa madai kuwa umekuwa ukiigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi chote cha miezi 6 ambacho huwa unakimbizwa nchi nzima.
Rais Magufuli amesema miongoni mwa sababu zinazosababisha mwenge huo usifutwe  katika kipindi chake ni kuwa,mwenge huo unachochea maendeleo ya nchi.
Kwa mjibu wa rais Magufuli,katika mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2017,viwanda 148 vyenye thamani ya shilini mia nne na sitini na nane vitakavyotoa ajira zaidi ya elfu kumi na na tatu vimezinduliwa nchi nzima.
Pia alisema anawashangaa wanaotaka mwenge huo ufutwe, kwani wao ndio huwa mstari wa mbele kupokea Kifimbo cha Malkia au kushiriki kwenye mwenge wa Olimpiki.
Sherehe  za kuzima mwenge wa uhuru zimesherehekewa sambamba na kilele cha wiki ya vijana pamoja na kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha baba wa taifa hayati Julius nyerere kilichotkea Oktoba 14 mwaka 1999.
‘’Kaulimbiyu kwa mwaka huu inasema shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA