SIMULIZI YA MAUAJI YA WANANDOA YALIYOTKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MKOANI KATAVI



Na.Issack Gerald-Tanganyika Katavi
WANANDOA Adamu Mtambo(41) na mkewe  Catalina  Mtambo(39 )wakazi  wa Kitongoji cha Kasekese  B  Kata ya  Kasekese wilayani Tanganyika   Mkoani Katavi  wameuawa  kwa  kukatwa mapanga wakiwa wamelala  chumbani kwao.

Afisa  Mtendaji wa Kata ya Kasekese Ramadhani Ibrahimu  alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jana majira ya saa 6:45 usiku nyumbani kwao.
Akielezea tukio hilo alisema kuwa marehemu  Adamu ambae  alikuwa ni  mfanya  biashara  anamiliki maduka  mawili  Kijijini   hapo  siku  hiyo  alifanya   biashara ya kuuza  duka  kama  ilivyo  kawaida  yake na  baada ya muda wa  kufunga duka  ulipofika alifunga na aliingia ndani  kulala  yeye na  mke wake.
 Wakati wakiwa  wamelala walikwenda wauaji hao  ambao wanasadikiwa kuwa walikua watatu na walifyatua risasi tatu za bunduki hewani ilikuwatisha majirani ambao wangefika kutoa miaada, kisha kuvunja  mlango  na kuingia  ndani ya chumba  moja kwa moja walichokuwa wamelala wanandoa hao.
 Afisa mtendaji huyo alisema  baada ya kuingia  chumbani waliwakuta wanandoa hao kitandani ndipo walipoanza kuwashambulia kwa kuwakata kata kwa panga katika sehemu za usoni na kichwani na  kuwashambulia  kwa kutumia malungu.
Wakiwa wanawapiga marungu mwanaume alijaribu kuwasihi waache na  na kuwaeleza kama shida yao ni fedha yupo  tayari kuwaonyesha  mahali zilipo lakini hawakuacha ndipo walipoanza kupiga makelele ya  kuomba msaada kwa  majirani.
Alisema  kutokana na kelele hizo ndipo watoto wa marehemu ambao  nao walikuwa wakiishi kwenye  nyumba  hiyo wakiongozwa na  kaka yao  aitwaye  Charles waliingia  chumbani kwa  wazazi wao kwa lengo la kutoa msaada  hata  hivyo walishindwa baada ya  kushambuliwa na watu hao kwa kupigwa marangu hali iliyowalazimu wakimbilie kwenye vyumba vyao vya kulala na kujifungua.
 Hata hivyo Majirani walifika  kwenye  eneo hilo na  kukuta  mlango wa  mbele ya  nyumba ukiwa umevunjwa na walipoingia  kwenye chumba walichokuwa wanalala marehemu hao waliwakuta wakiwa wamelala  chini ya kitanda huku wakiwa na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za miili yao huku damu zikiwa zimetapakaa  chumbani na wauaji kutorokea kusikojulikana.
Mwenyekiti wa  Kitongoji cha  Kasekese  Happnes Bona alisema jitihada za kutafuta usafiri kwa  ajiri ya kuwafirisha wanandoa  hao kuwapeleka hospitali ya wilaya ya Mpanda zilifanyika na wakiwa njia walifariki.
 Alisema toka  amekuwa mwenyekiti wa  Kitongoji hicho hajawahi kuona mauaji ya kutisha na yakikatili kiasi hicho kwani marehemu  hao waliuawa kwa kukatwa  katwa  kama wanyama.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda alipotafutwa majira ya saa 10 jioni ili kuelezea hatua ambazo zimechukuliwa na jeshi la polisi kutokana na tukio hilo,kamanda Nyanda alisema hana taarifa kuhusu mauaji hayo.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA