OPAREHENI YANUKIA WILAYANI TANGANYIKA, USALAMA KWA RAIA UTAKUWEPO?

DC Tanganyika Salehe Mbwana Muhando
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amewataka wananchi wanaoishi  Kalumbi katika kijiji cha Mpembe, Lyamgoloka katika eneo la ushoroba wa wanyama,Igalukilo, Bariadi na Misanga Wilayani humo  kuondoka haraka katika maeneo hayo. 

Ametoa Tamko hilo leo wakati na kusema kuwa  tayari muda uliokuwa umetolewa umekwisha.                                       
Muhando amesema wananchi wa  Bariadi,Igalukilo na Misanga wanatakiwa kurudi katika maeneo ya Luhafwe yaliyotengwa kwa ajili ya makazi yao huku Wananchi wa kalumbi wakitakiwa kurudi katika eneo la makazi la kijiji cha Mpembe.
Amesema kumekuwa na matukio ya uvamizi wilayani humo mengine yakihusishwa na silaha za moto jambo ambalo hutokana na watu kukaa katika maeneo yasiokuwa na Mamlaka kamili za utawala na hivyo wahalifu  kugeuza maeneo hayo kama sehemu ya kujificha.
Hata hivyo kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wakazi Wilayani Tanganyika kulalamika silaha za moto kutumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya raia katika zoezi la kuwaondoa wanaodiwa kuvamia maeneo ya hifadhi ambapo Oktoba 12 mwaka huu mtu mmoja aliuawa na vyombo hivyo kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa.
Wakati huo huo wiki iliyopita Mhando alisema wataendelea kutumia nguvu kuwaondoa wananchi wasiotaka kuondoka kwa hiari katika maeneo ya hifadhi za misitu.
Wakati huo huo kumekuwa kukiripotiwa matukio ya watu kuuwawa na watu wasiojulikana mkoani Katavi ambapo karibu vifo vine vimeripotiwa.  

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA