WAFANYABIASAHARA WA MITUMBA WALAANI KUONDOLEWA KWA NGUVU KATIKA SOKO LA MPANDA HOTEL-Septemba 2,2017

WAFANYABIASHARA wa mitumba katika soko la Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelaani kitendo cha kutaka kuondolewa katika maeneo ya biashara zao kwa kinachodaiwa kuwa hawaruhusiwi kufanya biashara katika eneo hilo.

Wakizungumza baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa wao hufanya biashara katika eneo waliloelekezwa na mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda hivyo wanashangazwa na kitendo cha migambo kufika katika eneo hilo leo asubuhi  na kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa soko hilo Bw. Elisha kangombe amesema anashanga zwa na kitendo hicho na kusema kuwa yeye kama kiongozi hakubaliani nacho.

Aidha makamu mwenyekiti huyo amesema kama uongozi unalenga kuwaondoa wafanyabiashara hao ni vyema kuwaondoa wote bila kufanya ubaguzi na kuwatafutia maeneo mbadala ya kufanya biashara zao.

 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA