MBUNGE MTEULE WA CUF AFARIKI DUNIA-Septemba 2,2017

Bi Hindu Mwenda
Mmoja wa wabunge walioteuliwa kuchukuwa nafasi za wabunge nane wa chama cha wananchi (CUF) waliovuliwa uanachama na mwenyekiti wa CUF,Bi Hindu Mwenda amefariki dunia.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki jana jioni baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo hajaeleza kiundani chanzo cha kifo chake lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa hapo baadaye.
Marehemu Bi Hindu ambaye amefarikia dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Marehemu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wapya waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba

Habari zaini ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA