RAIS UHURU KENYATTA ASEMA HAKUBALIANI NA MAAMUZI YA MAHAKAMA HUKU WILLIUM RUTO NAYE AKITAKA TUME YA UCHAGUZI KUTANGAZA TAREHE MPYA YA UCHAGUZI-Septemba 2,2017
![]() |
Naibu wa rais wa Kenya William Ruto |
Hatua ni baada ya Ijumaa mahakama ya juu zaidi kubatilisha
ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita,ikisema
kulikuwa na dosari kubwa zilizokiuka katiba ya Kenya.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeusifu uamuzi huo wa
mahakama,papo hapo alishutumu vikali tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC na pia
kuwalaumu waangalizi wa kumataifa kwa kile alichokitaja ' kuhalalisha
udanganyifu uliotokea na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.
Amewataka waliohusishwa na udanganyifu huo kujiuzulu ,
kufutwa kazi na hata kuchukuliwa hatua za kisheria wakisema kamwe hawawezi
kuaminiwa kusimamia uchaguzi ujao.
![]() |
Rais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakora |
Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta amesema japo anauhesimu
hakubaliani na uamuzi huo uliofutilia mbali ushindi wake na kwamba yuko tayari
kwa marudio ya uchaguzi huo unaotakiwa kufanyika katika kipindi cha miezi
miwili ijayo.
Habari zaidi
www.p5tanzania.blogspot.com
Comments