RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA NA WAUMINI KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO-Septemba 2,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo wameungana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato,Usharika wa Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam kusali Ibada ya Sabato.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania,Baba Askofu Mark Walwa Malekana aliyekuwa pamoja na Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati,Baba Askofu Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki,Baba Askofu Albert Nziku.
Akizungumza baada ya Ibada hiyo Mhe.Rais Magufuli amelipongeza Kanisa hilo kwa kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wake na pia kutoa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini na amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini katika kuwahudumia wananchi.
Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Usharika wa Magomeni Mwembechai.
Aidha pamoja na kuchangia Shilingi Milioni 1 kwa kwaya za Kanisa hilo na pia ameendesha harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa na kufanikisha kupata zaidi ya Shilingi Milioni ishirini na tano.
Kwa upande wake Baba Askofu Mark Walwa Malekana amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na kuchangia ujenzi wa kanisa.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA