MH.LOWASSA ATOA POLE KWA RAIS UHURU KENYATTA MAHAKAMA KUFUTA USHINDI WAKE-Septemba 2,2017

Mh.Edward Lowassa
Mjumbe wa kamati kuu ya (CHADEMA) na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ametoa pole kwa aliyekuwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kufutia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Urais uliofanyika Agosti 8 mwaka huu.


Mhe.Edward Lowassa amesema yeye bado ataendelea kumuunga mkono hata katika uchaguzi ujao kwa kuwa Uhuru Kenyatta ni kiongozi mwenye kusimamia Demokrasia na mwenye maono ambaye anaweza kuisadia Kenya.
Aidha Lowassa amesema kuwa anamuheshimu sana Uhuru Kenyatta kutokana na jinsi ambavyo anaheshimu Demokrasia na kudai katika kipindi chake cha uongozi siku zote amekuwa akilinda Demokrasia ya nchi hiyo na kufanya wabunge,vyama na kila mtu nchini humo kuwa na haki.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA