TRA MKOANI RUKWA YASAKA MAPATO KWA UDI NA UVUMBA YASHTUKIZA UKAGUZI WA MAGARI HASA YA MIKOANI-Septemba 2,2017-

MAMLAKA ya mapato TRA mkoani Rukwa imefanya msako maalumu kwa lengo la kukagua mabasi ya abiria pamoja na ya mizigo ambayo haijalipiwa kodi mbalimbali.

Akizungumza jana wakati akiongoza msako huo,Meneja msaidizi idara ya ukaguzi wa TRA mkoa huo,Amina Shamdas amesema mamlaka hiyo inashirikiana na kampuni ya Yono Auction Mart kufanya ukaguzi huo.
Amesema mamlaka hiyo imebaini wafanyabiashara wa usafirishaji wamekuwa hawadai lisiti zinazotolewa na mashine za EFD wakati wakinunua mafuta huku Magari mengi yakiwa na stika za za kughushi za kulipia Mapato.

Kwa upande wake David Philipo ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya Yono Action Mart ya mjini Sumbawanga amesema wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutoka kwa wafanyabiashara hao ambapo baadhi yao wamekuwa ni wakaidi katika kutii sheria.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA