WANAFUNZI 7 WAFARIKI DUNIA BAADA YA BWENI LAO KUTEKETEA KWA MOTO NCHINI KENYA-Septemba 2



WANAFUNZI saba wamefariki na makumi wengine wakijeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls mjini Nairobi.
Baadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo
Magari ya kukabiliana na dharura yalifilka katika shule hiyo mapema alfajiri ili kuswanusuru walioathirika
Maafisa wa polisi wakishika doria nje ya shule ya Moi Girls liliopo jijini Nairobi nchini Kenya


Waziri wa elimu Nchini Kenya Fred Matiang'i amesema kuwa wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini ambapo kwa mjibu wa madaktari  nchini humo wawili kati ya hao 10 wako katika hali mbaya huku wengine wanane hali zao zikiendelea vizuri.
Wakati huo huo kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba mwekundu katika shule hiyo kimesema takriban wanafunzi 10 hawajulikani waliko ambapo kufuatia hali hiyo  shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo ambapo tayari kundi la wataalam wa upasuaji ikiwemo madaktari wako katika shule hiyo kubaini chanzo.
Waziri Fred Matiang'I hata hivyo amesema wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.
Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com   

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA