RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMA ZA RAMBIRAMBI WALIOFARIKI AJALI YA BASI LA CITY BOY,ATOA MAAGIZO


Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya basi la kampuni ya City Boy iliyotokea jana Aprili 4,2018.
Katika ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Makomero Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora imesababisha vifo vya watu 12 na wengine 46 kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoa wa Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso la lori lililokuwa likitokea Singida kuelekea Igunga.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 5,2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli  mbali na kutoa pole,amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha,kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.
Rais amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri kufikisha salamu zake  za pole kwa wafiwa wote  na amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahala pema peponi huku akiwapombea majeruhi wapone haraka.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA