MKUU WA MKOA ASIKITISHWA WATOTO KUTORIPOTI SEKONDARI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesikitishwa na wazazi ambao hawajawapeleka shuleni watoto wao kujiunga na masomo ya sekondari kidato cha kwanza mwaka 2018 baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2017.

Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa masikitiko yake wakati akifungua vikao vya wadau wa elimu  Mkoani Katavi vikao ambavyo vinalenga kujadili,kutathimini  na kuchukua hatua dhidi ya vikwazo vinavyosababisha Mkoa wa Katavi kufanya vibaya katika ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2017 ukishuka kutoka nafasi 3 za juu kitaifa na kufikia nafasi ya 9.
Aidha Muhuga amesema mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu,wanafunzi wapatao 240 wilayani Tanganyika walikuwa hawajaripoti shuleni ambapo amewataka madiwani wawahamasishe katika kata zao wawapeleke shuleni watoto wao hata kama hana sare na utaratibu mwingine utaendelea baadaye kubainisha chanzo cha kukosa sare.
Aidha Mkuu wa Mkoa katika kupunguza changamoto ya uhaba wa miundombinu ya shule ya Mtakumbuka amechangia shilingi 500,000 kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto ya miundombinu ya shule ya msingi Mtakumbuka.
Kwa mjibu wa  mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msingi Mtakumbuka Bw.Augustino Paul Filimbi amesema shule hiyo yenye  matundu 6 ya vyoo matatu yakiwa ya wavaulana na mengine ya wasichana haina choo cha walimu huku vyumba vinne vya madara vilivyopo kati ya hivyo viwili kodondoka wakati wowote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Francis Nzyungu kupitia kikao hicho amesema wanaendelea kutumia fedha za wahisani mbalimbali wakiwemo P4R,Equip Tanzania na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ili kutatua changamoto ya miundombinu katika shule za Manispaa.
Vikao vya wadau wa elimu ambavyo vimezinduliwa jana katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na vinatarajia kufikia kilele chake Aprili 16 mwaka huu katika kijiji cha Majimoto Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele ambapo leo vikao hivyo vimeendelea katika Halmashauri ya Nsimbo.
Hata hivyo takwimu zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 2017 na Afisa elimu Mkoa wa Katavi Ernest Hinju zinaonesha wanafunzi zaidi ya 9000 mkoani Katavi wamekosa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA