WANAWAKE WAMZIKA MWANAMKE MWENZAO ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE KABLA NA BAADA YA KUFARIKI.



Wanawake wa mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,hatimaye wamefanya mazishi ya mwanamke mwenzao Rosemary Robert Ismail makazi wa mtaa huo aliyefariki dunia siku sita zilizopita baada ya kutelekezwa na mumewe Bw.Abdalla Ibrahim akiwa mgonjwa.
Wanawake hao wamesema wamefanya mazishi jana baada ya kupata kibali cha jeshi la Polisi Mkoani Katavi kinachowaruhusu kufanya hivyo baada ya ndugu zake kukosekana.
Katika hatua nyingine wanawake wanadai kutishiwa maisha na Bw.Abdalla Ibrahim kwa madai kuwa wameripoti kifo cha mwanamke mwenzao katika vyombo vya habari.
Kwa upande wa mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Mpanda Hotel Bi.Edita Nichoraus pamoja na mambo mengine amesema Bw.Abdalla Ibrahim ataitishwa kuanzia kesho Machi 14 ili kujibu tuhuma za vitisho vya maisha anavyovielekeza wa wanawake walioshiriki mazishi.
Rosemary Robert Ismail anadaiwa kufariki Machi 7 mwaka huu na amezikwa juzi ambapo Bw.Abdalla Ibrahim awali katika mazungumzo na Mpanda Radio alisema marehemu hakuwa mkewe.
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA