CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA HATIHATI KUSITISHA KUDAHILI WANAFUNZI



CHUO cha ualimu cha Sumbawanga kilichopo mkoani Rukwa huenda kikasitisha kudahili wanafunzi ajili ya kujiunga na chuo hicho baada ya Kanisa katoliki jimbo la Sumbawanga kudai majengo yake baada ya serikali kutowapatia majengo mengine kama walivyoahidiana.
Katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC hivi karibuni alisema majengo yanayotumiwa na chuo hicho ni mali ya kanisa katoliki ambalo liliyatoa kwa serikali mwaka 1974 ili yatumike kama ofisi za mkoa wakati Mkoa huo ulipokuwa mpya na ukiwa hauna Ofisi.
Alisema kipindi hicho alikuwepo Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Sumbawanga marehemu Karolo Msakila ambaye aliombwa majengo hayo ili yatumike kama ofisi za mkoa huo ambapo alikubali na kuiazima serikali na ofisi za mkoa huo zilikuwa hapo.
Ilipofika mwaka 1989 serikali ya mkoa huo ukawa umejenga ofisi zake lakini haukuyarudisha majengo hayo kwa mmiliki wake ambaye alikuwa anataka kufungua chuo cha kilimo na badala yake serikali ilianzisha chuo cha ualimu bila makubaliano yoyote.
Baada ya muda mrefu kanisa katoliki liliyahitaji majengo yake ambapo serikali ya mkoa iliahidi kulipatia majengo yalikuwa yakitumika na kampuni ya ujenzi ya barabara kwa kiwango cha lami  kati ya Sumbawanga-Tunduma lakini hata hivyo serikali ya mkoa huo haikulipa kanisa majengo hayo badala yake yakatumika kuanzisha tawi la chuo cha Sayansi cha Mbeya(MUST).
Kutokana na hali  hiyo kanisa katoliki lilihoji kuhusu hatma ya majengo yao ambapo serikali ya mkoa iliahidi tena kulipa majengo ya kambi ya ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Mpanda yaliyopo katika eneo la Makutano mjini Sumbawanga, lakini pia haikuwa hivyo baada ya serikali kuweka ofisi za Tanroad mkoa na hivyo kanisa kukosa majengo hayo.
Baada ya kushindikana mara mbili zote kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga lilikutana na uongozi wa serikali ya mkoa ambapo lilisema halitaki tena kupewa majengo mengine bali wanataka majengo yao kwa kuwa kanisa hilo limevumilia na kufikia mwisho.
Kutokana na kujuwa majengo hayo si mali ya serikali kwa muda mrefu yalikuwa hayafanyiwi ukarabati mpaka hapo NACTE ilipotishia kukifunga chuo hicho kutokana na kuwa kimechakaa, ndipo serikali ya mkoa ilipoliomba tena kanisa katoliki liwape muda ambapo lilitoa miaka mitano wanafunzi hao wawe wameondoka katika majengo yao na serikali ya mkoa iwe imejenga chuo chake na wakabidhi majengo kwa kanisa hilo liendelee na matumizi waliyokusudia wakati yakijengwa.
Mkuu wa Mkoa wangabo aliwaambia wajumbe wa kikao cha RCC serikali ya mkoa imewasiliana na tasisi ya Jumuiya ya Maendeleo mkoani Rukwa (JUMARU) ambapo imetoa ardhi katika kijiji cha Pito nje kidogo ya mji wa Sumbawanga ambapo yalikuwa mashamba ya bega kwa bega yanayomilikiwa na kijiji hicho ambapo serikali ya mkoa imeanza mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ualimu Sumbawanga.
Alisema lengo la serikali ya mkoa ni kujenga chuo hicho na kwa kuwa eneo ni kubwa kijengwe pia chuo kikuu ambacho kitamilikiwa na serikali ambacho kitakuwa makao yake makuu mkoani Rukwa.
Baada ya taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti huyo wa RCC, wajumbe wa kikao hicho walishauri kuwa ni vizuri pia ukarabati ukaendelea kufanyika katika chuo hicho kinachotumika hivi sasa kilichopo eneo la Kantalamba ili NACTE wasisitishe kuwapangia wanafunzi kwa kua miaka mitano waliyo azimwa na kanisa hilo bado ni kipindi kirefu.
Chanzo:Rukwa kwanza Bolg
Habari zadi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA