RAIS MAGUFULI AWAONYA TRA
Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza
Kamishna wa TRA,Waziri wa Fedha na katibu mkuu kwenda kuishughulikia Shirika la
Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kuacha tabia zake chafu za kuwaongezea raia
kodi za mapato pindi wanapokwenda kupata huduma hizo.

Pamoja na hayo,Dkt. Magufuli
ameendelea kwa kusema "TRA muangalie kodi zenu mnazozitoza, inawezekana
nyingine ni kubwa mno kuliko miradi wanayotekeleza wananchi badala ya kuwa
motisha kwa walipa kodi inakuwa kero kwao na badala yake wanabuni njia ya
kukwepa kulipa kodi.
Kwa upande mwingine,Dkt. Magufuli
ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya mlipa mkodi kwa wananchi ili kuweza
kuwapa uelewa wanachi na waweze kulipa kodi kwa heshima kwa taifa lake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments