RUKWA BADO WALIA NA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA


MKOA wa Rukwa bado unakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo jumla ya vyumba 4,226 vinakitajika ili  kumaliza tatizo hilo.
Afisa elimu mkoa huo Nestory Mroka alisema mahitaji hayo yamekuwa yakisababisha mkoa huo kutopiga hatua katika mafanikio ya elimu.
Alisema ili wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao ni lazima kuwe na miundombinu mizuri,walimu wa kutosha,vitabu pamoja na walimu lakini kama kuna mapungufu kati ya hayo mambo hata ufaulu hauwezi kuwa mzuri.
Aidha Mroka alisema kutokana na changamoto hizo jitihada za makusudi zinahitajika katika kulimaliza tatizo hilo pamoja na mengine ili kuinua ufaulu wa wanufunzi katika shule za msingi pamoja na sekondari ambapo mpaka sasa ufaulu katika kidato cha nne ni wastani wa daraja la nne.
Wakati huo huo,Afisa elimu huyo alisema yeye binafsi amejitahidi kuhakikisha anawasimamia walimu ili watimize wajibu wao ipasavyo ikiwamo kuwepo kazini kwa muda mwafaka sambamba na kufundisha kwa juhudi zote ili idara ya elimu iwe mfano wa kuigwa kwa kufanya vizuri mkoani humo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo aliziagiza halmashauri zote za mkoani humo kuhakikisha zinakuja na  mikakati ya kumaliza tatizo hilo pamoja na kwamba limeongezeka baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya elimu bure.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa hivi sasa serikali inajikita katika uchumi wa viwanda lazima pia kuhakikisha kuwa elimu haibaki nyuma na mzizi wa kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza vizuri katika elimu kwani huko ndiko watapatikana wataalamu watakao fanya kazi katika viwanda hivyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA