WANANCHI WATAKA ELIMU YA USALAMA BARABARANI MPANDA

Wananchi katika halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoa katavi wamelitaka jeshi la polisi kutoa elimu juu ya alama za barabarani ili kupunguza ajali .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumiaji wa barabara wamesema elimu ya usalama barabarani itawasaidia watembea kwa miguu kujiepusha na ajali za mara kwa mara zinazotokea kwa kutokujua matumizi ya alama hizo.

Kamanda wa usalama barabarani mkoa Katavi John Mfinanga amesema elimu ya usalama barabarani na matumizi ya alama wanazitoa kupitia radio na katika vijiwe vya bodaboda ili kuwasaidia watembea kwa miguu kuweza kuzifahamu sheria na alama hizo.

Mfinanga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi pindi semina hizona kusema kwamba semina hizo zinatolewa bure na hazina malipo.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA