THAMINI UHAI WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA MKONI KIGOMA

Shirika la Thamini uhai limejitolea dawa na vifaa tiba takribani aina 50 katika vituo vya afya 46 ndani ya mkoani Kigoma huu vyenye thamani ya shiling million 127 lengo likiwa ni kusaidia vituo hivyo kutoa huduma stahiki na kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo daktari Bingwa wa magonjwa ya akina mama ya uzazi kutoka shirika hilo Dkt.Sande Dominick amewataka watoa huduma kutumia dawa na vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwa.
Kwa miaka kadhaa sasa idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya imeongezeka kutoka asilimia 38 hadi kufikia asilimia 60 yote ni kutokana na jitihada za mashirika binafsi ambapo  Meneja mahusiano na mawasiliano kutoka shirika la thamini uhai Viktoria Marijani amesema wamekuwa wakifanya hivyo ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Akimwakilisha Kaimu katibu tawala Mkoani Kigoma mhandisi Aziz Mtabuzi,Dkt Lameck Mdengo ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake baada ya kupokea msaada huo ametoa shukrani Kwa niaba ya serikali na kutoa rai kwa vituo vya afya vyote 46 kutumia msaada huo kama ilivyotarajiwa.
Hata hivyo bado serikali inaalika wafadhili wengi kufika na kufadhili shughuli za miradii ili kuhakikisha huduma za afya zinakuwa endelevu mkoani  Kigoma lakini pia kupanua wigo wa kufadhili katika mkioa mingine ya Tanzania.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA