RAIS MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE WA PAUL KAGAME AAGANA NA BALOZI WA ZIMBABWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli jana amekutana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Rwanda na aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.Donald Kaberuka na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU).
Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa Dkt.Kaberuka amesema uchumi wa Tanzania unakua vizuri na amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa jinsi anavyosimamia ukuaji wa uchumi huo.
Dkt.Kaberuka amesema katika mazungumzo hayo pia amewasilisha ujumbe wa Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame ambaye kuanzia mwezi huu atakua Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na ndiye aliyekabidhiwa majukumu ya kufanya mabadiliko ndani ya umoja huo.
Wakati huo huo,Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini anayemaliza muda wake Mhe. Edzai Chimonyo na kumpongeza kwa uwakilishi mzuri alioufanya kwa miaka 10 aliyoiwakilisha Zimbabwe hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa,Mhe.Rais Magufuli amemuomba Mhe.Chimonyo kumfikishia salamu za pongezi Mhe.Emmerson Mnangagwa kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zimbabwe na amemuhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri wa kihistoria na kidugu uliopo kati yake na Zimbabwe.
Mhe Chimonyo ameshukuru kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chake cha Ubalozi hapa nchini na amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa namna anavyoiongoza nchi huku akitaja baadhi ya mambo yanayofanywa kwa mafanikio makubwa kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa,ujenzi wa miundombinu hususani barabara,madaraja na viwanja vya ndege.
Mhe.Chimonyo ambaye alikuwa kiongozi wa Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Kaimu Kiongozi wa Mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania amesema Mabalozi hao wanafurahishwa na wanaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mhe.Rais Magufuli ikiwemo kuhamia makao makuu Dodoma.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA