MAAMUZI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR

KAMATI ya Ulinzi na Usalama  Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman imelazimika kutengua makubaliano ya zamani ya uchukuaji wa mizigo katika bandari ya Wete. Kamati hiyo imesema imetengua makubaliano hayo baada ya kubaini  kuwepo na mgogoro kati ya vikundi vya uchukuzi bandarini hapo.
Vikundi vya uchukuzi ambavyo vilikuwa katika mgogoro wa uchukuzi  wa mizigo bandarini hapo ni Shikamana na Dausheni ambapo makubaliano hayo yalikuwa ni kwa wanachama wa Shikamana kubeba mizigo kwenye meli wakati Dausheni kubeba mizigo inayoingia bandarini hapo kwa njia ya majahazi  .
Baada ya kufuta maamuzi hayo,Serikali imeutaka uongozi wa Shirika la bandari Tawi la Pemba kusimamia mgawanyo sawa wa uchukuzi wa mizigo  wa meli na majahazi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA