VIWANDA VYA MWATEX NA KEKO VIMEPEWA SIKU 14 VIZALISHE BIDHAA

Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha jijini Mwanza na cha dawa cha Keko jijini Dar es Salaam kuanza uendeshaji wa kiuzalishaji.
Amesema kinyume cha hilo,viwanda hivyo vitataifishwa na kurejeshwa kwenye umiliki wa umma.
Rais Magufuli amesema hayo jana alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza.

Amesema Serikali imechoka kusikia kauli na maelezo ya “tuko kwenye mchakato” zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango kinachostahili.
Rais ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa kiwanda cha Mwatex kinafanya kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji.
Akizungumzia ujenzi wa kiwanda cha dawa,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu.
Mwalimu amesema katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda,wizara kwa kushirikiana na wadau wanakamilisha mchakato wa kujenga kiwanda cha dripu na bidhaa zingine za hospitali mkoani Simiyu.
Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya,amesema Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya Sh7.1 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba na dawa.
Amesema jitihada zinaendelea ili kuipatia Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure mashine ya CT-Scan.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA