MH.ZITTO AMEPEWA DHAMANA

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015.
Mwanasheria amesema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani.
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo.
Mbali na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na viongozi wa chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa udiwani na kusema endapo wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho kitakuwa faraja kwao.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA