MASOKO YA USIKU MKOANI KIGOMA,HOFU USALAMA IMETANDA

Imeelezwa kuwa Masoko ya usiku katika baadhi ya kata za wilaya ya Buhigwe mkoani kigoma,yanapalekea matatizo kwa wakazi wa wilaya hiyo,yakiwemo matatizo ya kiusalama kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.
Diwani wa kata ya Mkatanga ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Bw.Hamiss Lukanka  amesema soko hasa lililoko katika kata ya Mkatanga linapelekea hata watoto wa shule kutokupata muda wa kujisomea kutokana kutumia muda wao mwingi hasa wa usiku kuzurula sokoni humo.
Amesema mpaka sasa wana mpango wa kuratibu na kusimamia soko hilo liwe linaanza muda wa asubuhi kwa siku maalum,ili kuondokana na changamoto zinazotokana na masoko ya usiku na kutoa nafasi kwa wakazi wa vijiji jirani kuleta bidhaa zao katika soko hilo.
Katika upande mwingine Bw.Lukanka amewataka wananchi wa wilaya ya Buhigwe kufanya kazi kwa kushilikiana Bila kujali utofauti wa vyama wilayani humo,lengo kubwa  likiwa ni kuleta maendeleo ya wilaya yao.
Chanzo:Grol Paschal,Mhariri-Issack Gerald

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA