MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA AMERUHUSU AJIRA ZA MUDA

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata.

Amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo.

Katika hatua nyingine amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea upungufu wa watendaji hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa na sakata la watumishi wenye vyeti feki.

Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga alitoa agizo kwa vijiji na mitaa kuajiri watumishi wa muda wakati wakisubiri serikali kuu kutangaza ajira.

Baraza la Madiwani limeendelea jana ambapo Madiwani wamewasilisha mapendekezo mbalimbali ya utekelezwaji wa bajeti katika kata zao.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA