TFS WAMETOA ONYO KWA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI

Wakazi mkoani katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia misitu na kufanya shughuli katika hifadhi zinazoharibu uoto wa asili.
Kauli hiyo imetolewa na Samwel Matula ambaye meneja wa misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi ambapo amesema hakuna ruhusa ya watu kufanya shughuli kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo meneja misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi amewataka wote walioondolewa katika maeneo ya misitu kufuatia operesheni iliyofanyika mwezi wa saba mwaka huu ,kutorudi katika maeneo hayo na sheria kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo.
Mwezi Julai mwaka huu,operesheni ya kuwaondoa watu katika maeneo ya misitu kama vile msitu wa msaginya ,na misitu north east mpanda ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu iliyopo Katavi kwa manufaa ya wananchi wote.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA