WANANCHI WILAYANI TANGANYIKA WAMETAKIWA KUWASILISHA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI BADALA YA KUJENGA KIHOLELA

Na.Issack Gerald-Tanganyika
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa wito kwa wakazi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha malalamiko yao kuhusu migogoro ya ardhi badala ya kuamua kujenga kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa idara ya ardhi na maliasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bi.Josephine Beda Lupia wakati akizungumzia kuhusu mikakati iliyowekwa kudhibiti wakazi wanaojenga makazi holela katika maeneo yasiyo rasmi.
Aidha Bi.Lupia amesema katika kuweka matumizi bora ya ardhi,halmashuari kwa kushirikiana na baraza la madiwani katika halmshauri hiyo,walipitsha kutengwa zaidi ya  hekta 46,000 kwa ajili ya sekta ya kilimo,uwekezaji na ufugaji.
Katika hatua nyingine Bi.Lupia amesema katika mpango bora wa ardhi,walizingatia pia haki za makundi maalumu yasiyokuwa na uwezo kwa kulipia fedha taslimu na badala yake wakapewa nafasi ya kulipa kwa awamu ambapo jumla malipo yalikuwa hadi shilingi laki moja kwa kiwanja.
Maeneo yaliyokuwa yakitajwa kuvamiwa na wakazi kuendesha shughuli mbalimbali bila kuidhinishwa kuwa makazi rasmi ni pamoja Misanga,Lyamgoroka na Mnyamasi.
Habari zaini ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA