CWT MKOANI KATAVI KIMEZUNGUMZIA SHULE ZA SERIKALI KUFANYA VIBAYA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA 2017.



Na.Issack Gerald-Katavi
CHAMA cha walimu Tanzania CWT mkoani Katavi kimesema wanafunzi wengi wa shule za serikali wanashindwa kufaulu vizuri kwa kiwango cha juu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi wengi darasani kwa wakati mmoja.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa CWT Mkoani Katavi Hamisi Ismail ambapo amesema shule za binafsi zinafanya vizuri katika kufaulisha wanafunzi kutokana na kuwa na idadai ndogo ya wanafunzi darasani idadi ambayo ni rahisi mwalimu kuimudu anapokuwa anafundisha suala ambalo limekuwa gumu upande wa shule za serikali.
Katika hatua nyingine amesema uwepo wa vitabu vingi vyenye mitaala inayotofautiana husababisha wanafunzi kuelewa mambo tofauti akisema kuwa ni vema serikali ikawa na kitabu kimoja kitakachotumika nchi nzima.
Wakati huo huo Mwalimu Hamisi Ismail amesema chama cha walimu CWT mbali na kuwepo kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya walimu,pia kinahakikisha walimu wanawajibika katika kufundisha wanafunzi ipasavyo pamoja na kuzingatia maadili mema.
Kauli ya chama inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Baraza la Mitihani Tanzania NACTE kutangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba ambapo imeonekana shule za serikali zimefanya vibaya kuliko shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA