RAIS MAGUFULI AMEPOKEA HATI 3 ZA MABALOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea hati za utambulisho za Mabalozi watatu waliopangiwa kuziwakilisha nchi za Oman,Uholanzi na China hapa nchini.
Rais dkt John Pombe Magufuli
Waliowasilisha hati zao kwa Mhe.Rais Magufuli,Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe.Ali Abdullah Al Mahruqi – Balozi wa Oman hapa nchini,Mhe. Jeroen Verheul – Balozi wa Uholanzi hapa nchini na Mhe.Wang Ke – Balozi wa China hapa nchini.
Mhe.Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itafanya kazi nao kwa ukaribu ili kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania hususani katika uchumi.
Mhe. Rais Magufuli amemuambia Balozi Jeroen Verheul wa Uholanzi kuwa Tanzania inayo gesi nyingi na itafurahi kupokea wawekezaji kutoka Uholanzi ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na teknolojia kubwa katika sekta hiyo.
Kwa upande wa Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke,Mhe.Rais Magufuli amesema uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria na kidugu, hivyo ametoa wito kwa Balozi huyo kuuendeleza na kuhakikisha fursa zenye manufaa kwa nchi zote zinatumiwa ipasavyo ikiwemo kukuza uwekezaji, biashara,utalii na ushirikiano katika usafiri wa anga.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA