KAULI YA KAMANDA WA POLISI TABORA HII ITAZAA MATUNDA?AU NI DANGANYA TOTO?




Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Tabora ACP Wilbrod Mutafungwa amewataka wananchi waliokimbia hivi karibuni kwenye kijiji cha Mwamabondo kurejea katika makazi yao.
Wakazi hao walikimbia kufuati msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi  baada ya wananchi hao kufanya jaribio la  kutaka kuwaua wanawake wanne waliowapiga na kuchomwa moto sehemu za siri kutokana na imani za kishirikina.
Aidha Kamanda Wa Polisi Mkoani Tabora Amelazimika Kusafiri Umbali Mrefu Wa Zaidi Ya Kilometa 150 Kwa Ajili ya Kuzungumza na baadhi ya wananchi  waliobakia Kijijini Hapo.
Wakati akizungumza na wananchi hao miongoni mwa mambo yaliyojitokeza Katika Mkutano huo ni pamoja na kuelezwa kuwa Mahudhurio ya wanafunzi wa shule ya msingi kijijni  hapo yameshuka kwa asilimia 30 kutokana na wazazi wa wanafunzi hao kukimbia kutakimbia makazi yao.
Miongoni mwa Wanawake wanne walionusurika kifo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuokoa maisha yao.
Mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu wananwake 4 wakazi wa kijiji cha Mwamabono wilayani Uyui walinusurika kufa baada ya kupigwa na kuchomwa moto sehemu zao za siri kutokana na imani za kishirikina wakidaiwa kuhusika na kifo cha mganga mmoja kijijini hapo.
Hiki ni Kijiji Cha Mwamabondo Kilichopo Kata Ya Loya Wilayani Uyui Mkoani Tabora,wakazi wake Wanajishughulisha Zaidi na shghuli za kilimo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA