Posts

RPC KATAVI : JESHI LA POLISI LIMEJIANDAA KUWADHIBITI WAANDAMANAJI OPARESHENI UKUTA,VYAMA VILIVYOKUWA VIMEPANGA KUANDAMANA VYAAHIRISHA MAANDAMANO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi JESHI la Polisi Mkoani Katavi lilikuwa limesema limefanya maandalizi ya kutosha kuwadhibiti watu,kikundi au vyama vya siasa ambavyo vingefanya maandamano kesho Septemba mosi. Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam ACP Damasi Nyanda Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 31,2016                                           

RPC NYANDA KATAVI LEO KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI.

Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ASP Damasi Nyanda leo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Mkoani Katavi kuzungumzia mandamano ya Opareshen Ukuta yanayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

WAFANYABIASAHARA MANISPAA YA MPANDA WAPEWA SIKU 6 KUONDOKA MASOKO YASIYO RASMI KABLA YA NGUVU KUTUMIKA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda WANANCHI wanaofanya biashara katika masoko yasiyo rasmi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kuondoka na bidhaa zao wenyewe kwa hiari kabla ya Septemba 5 mwaka huu kuondolewa kwa nguvu. Katika Picha Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu(PICHA NA.Issack Gerald) Miongoni mwa wafanyabishara wanaopigwa marufuku soko lisilo rasmi lililopo Ujenzi Machinjioni Mpanda hotel.                                                    

MKUU WA WILAYA TANGANYIKA AONYA WATAKAOANDAMANA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI,ASEMA OPARESHENI UKUTA IWE NI KUJENGA MADARASA,KUTENGENEZA MADAWATI NA SHUGHULI NYINGINE ZA MAENDELEO.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Saleh Mbwana Mhando,ametoa onyo kwa wananchi na wanachama wa vyama vya siasa watakaofanya maandamano ya Opareshen Ukuta katika Wilaya hiyo yanayotarajia kuanza Septemba mosi.  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyiika Saleh Mhando                                        

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKAZA MWENDO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE

Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh.Saleh Muhando ameahidi kulishughulikia swala la mgogoro wa ardhi katika eneo la Lyamgoroka eneo ambalo linaonekana kuwa limeuzwa na   mwenyekiti wa kijiji hicho    kinyume cha sheria ya ardhi.

WANAUME WATAJWA KUWA MIONGONI MWA SABABU ZINAZOCHANGIA KUONGEZEKA VVU KATAVI

  Na.Richard Sokoni-Mpanda Imebainika kuwa   ongezeko la   maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU) kunatokana   na   baadhi ya mwanaume   kutojitokeza kupima afya zao sanjari na wenzi wao .

VIJANA WATII AGIZO LA MKURUGENZI WA MANISPAA KUTOSAFISHA VYOMBO VYA USAFIRI KATIKA VYANZO VYA MAJI

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Vijana na watu waliokuwa wakitumia mto Mpanda eneo la daraja linalotenganisha Kata ya Mpanda Hotel na Misunkumilo kusafisha magari na vyombo vingine vya usafiri,wamesitisha shughuli hiyo kutii agizo la mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda akiwataka kutofanya shughul hiyo kwa lengo la kulinda vyanzo vya maji.