MWANAMKE ASIYEJULIKANA ATUPA MTOTO WA UMRI WA SIKU 1 KATIKA UWANJA MICHEZO


Mtoto wa jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa na umri wa  siku 1 ameokotwa akiwa hai katika uwanja wa Azimio  Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya kutupwa  na mwanamke ambaye mpaka sasa hajafahamika majina wala makazi yake.
Mashuhuda wa tukio wakilaani tukio hilo,wamesema mtoto huyo inasadikiwa alitupwa Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu majira ya mchana mpaka alipookotwa majira ya saa kumi  jioni .
Hata hivyo wananchi wilayani Mpanda wamesikitishwa na tukio hilo na kuomba  hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika kutenda unyama huo dhidi ya mtoto asiyekuwa na hatia.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii manispaa Redgunda Mayorwa amethibitisha kupokea taarifa za mtoto huyo ambapo amesema jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumpata na kumfikisha katika vyombo vya sheria mwanamke aliyetenda unyama huo.
Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa kitendo cha kutupa mtoto hakina tija kwa jamii na amewashauri wanawake kuwa kama hawawezi kuzaa basi watumie uzazi wa Mpango kuliko kutesa mtoto.
Mtoto huyo ambaye jina lake ni FURAHA kwa mjibu wa barua ya mwanamke huyo aliyoiacha karibu na mtoto huyo alipokuwa amelazwa uwanjani,mpaka sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Hilo siyo tukio la kwanza kwa wanawake wa Manispaa ya Mpanda kutupa watoto huku wahusika wakiwa hawakamatiki.
Mengi Zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA