Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima amepokea madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni saba na nusu ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za Wilaya ya Mpanda.
MKUU wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,amezitaka Halmashauri zote za mkoa wa Katavi kutenga fungu katika bajeti zake na kuzilipia kaya maskini ili zinufaike na mfuko wa jamii CHF.
Na.Issack Gerald-Katavi Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamehakikishiwa kulipwa asilimia 100 ya uuzaji wa zao hilo, kwa msimu wa mauzo ya 2015/2016.
Wakazi wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,wamemwomba Mkuu wa Wilaya kumaliza tatizo la upimaji waardhi katika mtaa huo ambalo limedumu kwa kipindi kirefu bila kupatiwa ufumbuzi.
MTU Mmoja Mkazi wa Mji wa Zamani Katika Manispaa ya Mpanda amefikikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mjini Mpanda kwa Kosa la Kuua bila Kukusudia.