MGOGORO WA ARDHI MTAA WA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA WAENDELEA KUTOKOTA,WANANCHI WAMWANGUKIA MKUU WA WILAYA



Wakazi wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,wamemwomba Mkuu wa Wilaya kumaliza tatizo la upimaji waardhi katika mtaa huo ambalo limedumu kwa kipindi kirefu bila kupatiwa ufumbuzi.

Wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa kwa muda mrefu sasa,wamekuwa wakihaha zaidi namna gani waishi kwa amani bila bughudha yoyoye inayohusiana na migogoro ya ardhi inayolenga upimaji.
Kutokana na wakazi hao kupaza sauti zao na wakati mwingine bila kusikilizwa kwa mjibu wa madai yao,hatimaye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikaamua kufika eneo la mgogoro kupata zaidi kero za wananchi juu ya maeneo yao kwa njia ya kufanya mkutano wa hadhara.
Pamoja na mambo mengine wakazi hao wa mtaa wa Nsemulwa wakamwomba Mkuu wa Wilaya kumaliza tatizo la upimaji wa ardhi katika mtaa huo tatizo ambalo limedumu kwa kipindi kirefu bila kupatiwa ufumbuzi.
Kupitia kikao cha hadhara kati ya Uongozi wa Wilaya ya Mpanda na idara za ardhi Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Nsemulwa wananchi wakapewa fursa ya kueleza madai yao.
Kutokana na baadhi ya wananchi kueleza kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama ya upiamji wa ardhi sanjari na kupatiwa hati miliki,imemlazimu Mkuu wa iadara ya Ardhi,mpango mji na maliasili Manispaa ya Mpanda Bw.Peter Makalipa kutoa ufafanuzi juu ya gharma ambapo amesema kuwa punguzwa kwa gharama za upimaji na hati ya kiwanja litapelekwa katika mamlaka husika ili lipitiwe upya kama ambavyo wananchi wameomba.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amewataka wananchi wenye malalamiko juu ya viwanja vyao kufika Ofisini ili madai yao yashughulikiwe kwa wakati na kwa mjibu wa sheria.
Kwa mjibu wa wananchi hao zaidi ya 800 wenye mgogoro wa ardhi katika mtaa wa Nsemulwa,mgogoro huo umedumu kwa takribani miaka mitano mpaka sasa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA