HALMASHAURI KATAVI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI KUSAIDIA KAYA MASKINI BIMA YA AFYA


MKUU wa mkoa wa Katavi Meja  Jeneral Mstaafu  Raphael Muhuga,amezitaka  Halmashauri zote za mkoa wa Katavi kutenga fungu katika bajeti zake na kuzilipia kaya maskini ili zinufaike na mfuko wa jamii CHF.

Rai hiyo ameitoa leo katika uzinduzi wa mfuko huo uliozinduliwa katika kijiji cha Kakese mbugani Manispaa ya Mpanda  mkoani hapa.
Aidha Muhuga amesema  kila mwananchi anatakiwa kujiunga  na mfuko huo ili kupunguza gharama za matibabu wanapopatwa na maradhi wanapokuwa hawana fedha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mfuko huo Kitaifa Bw.Eugen Mikongoti,ameupongeza Mkoa wa Katavi kwa kushika nafasi ya 5 kitaifa kwa uchangiaji wa Mfuko huo wa jamii.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kakese waliojitokeza katika uzinduzi huo ,wamepongeza hatua ya viongozi wa mfuko wa bima ya afya kuwafikia katika maeneo hayo kutoa elimu ya faida ya kujiunga na bima na hasara ya kutojiunga na mfuko huo.
Aidha Mkurugenzi wa mfuko huo Kitaifa Bw.Eugen Mikongoti,amewataka wakati wa Mkoa wa Katavi kwa ujumla kutambua kuwa kujiunga katika mfuko ni tahadhari ambayo itamsaidia kupatiwa matibabu kwa urahisi na gharama ndogo.
Mwandishi:Vumilia Abel
Mhariri : Issack Gerald
Endelea kufuatilia P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA