MKUU WA WILAYA YA MPANDA APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100.


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima amepokea madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni saba na nusu ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za Wilaya ya Mpanda.

Msaada wa madawati hayo umetolewa leo na Chama cha msingi cha ushirika Mpanda Katai ambapo msaada huo umekabidhiwa na Amani Rajabu Ambaye ni Meneja wa Chama hicho.
Akizungumza katika makabidhiano hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi za Chama hicho,Bw.Mwamlima pamoja na shukrani kwa msaada huo,pia ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano huo.
Katika mgawanyo wa madawati hayo,Halmashauri ya wilaya ya Mpanda itapata madawati 50 huku Manispaa ya Mpanda pia ikipata madawati 50.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ameagiza kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa madawati hayo.
Katika hatua nyingine,amewaagiza wakurugenzi wa Halmshauri za Wilaya na Manispaa ya Mpanda kuhakikisha hakuna utoro mashuleni kabla ya kuendesha oparesheni ya kusaka wanafunzi watoto.
Mwandishi:Esther Lameck
Mhariri :Issack Gerald
Endelea kufuatilia P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA