Posts

WANNE MBARONI KATAVI AKIWEMO MWENYE NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.60

Na.Issack Gerald-MLELE Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya wanyama Pori (TANAPA) ,linawashikilia watu wanne akiwemo mmoja ambaye amekamatwa na jino moja na mikia miwili ya Tembo vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 60.

WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KATAVI WATAKIWA KUEPUKA MAZINGIRA YA UKATIRI

Na.Issack Gerald-MPANDA . WANAFUNZI wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Katavi wametakiwa   kuepuka mazingira yanayopelekea   vitendo ya ukatili na unyanyasaji na   kuzingatia masomo.

WAKALA WA VIPIMO TANZANIA KUZINDUA MATUMIZI YA VIPIMO KESHO MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald-MPANDA Wakala wa vipimo Tanzania Kesho wanatarajia kuzindua na kukopesha mizani kwa wafanyabiashara wadogo Mkoani Katavi kwa ajili ya kuondokana na hasara zinazotokana na kuuza bidhaa mbalimbali pasipo kutumia vipimo halali.

UONGOZI HOSPITALI YA WILAYA MPANDA WALALAMIKIWA KWA KUTOA HUDUMA DUNI KWA WAGONJWA

Na.Issack Gerald-MPANDA BAADHI ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda wameulalamikia uongozi wa hospital ya wilaya ya Mpanda kwa kutoa huduma isiyoridhisha.

WAKAZI KATAVI WATAKIWA KUWA TAYARI KWA USAFI DESEMBA 9

Na.Issack Gerald-MPANDA. WAKAZI Katika Mkoa wa Katavi wametakiwa Kuwatayari Kushiriki Katika zoezi la Kufanya usafi wa Mazingira litakalofanyika Nchi nzima December 9 Mwaka huu.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA POLISI

Na.Mwandishi wetu-Mwanza. Mahakama kuu kanda ya mwanza imetupilia pingamizi la  polisi kuzuia  waombolezaji kufanya ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa geita Afonce Mawazo aliyeuwawa nov.14 mwakahuu kwa kukatwa mapanga.

WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WALIA NA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA

Na.Issack Gerald-MPANDA Wakazi wa kata ya Makanyagio katika Manispaa ya   Mpanda Mkoani katavi wameiomba mamlaka ya maji safi na salama Manispaa ya Mpanda kutafuta ufumbuzi wa kuondoa kero ya kukosekana kwa maji safi na salama kwa wananchi hao.