WANNE MBARONI KATAVI AKIWEMO MWENYE NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.60


Na.Issack Gerald-MLELE
Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya wanyama Pori (TANAPA) ,linawashikilia watu wanne akiwemo mmoja ambaye amekamatwa na jino moja na mikia miwili ya Tembo vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 60.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amemtaja ambaye amekamatwa na nyara hizo za serikali kuwa ni Haruna Exavery (20) mkazi wa kata ya Sitalike.

Aidha Kidavashari amesema,wamewakamata Juma Kapongo (55),Amos Gerald Kapongo (20) na Haruna Exavery Sikazwe(20), wote wakazi wa Kata ya Sitalike wakiwa na silaha moja aina ya gobore yenye risasi moja kinyume na sheria.

Mbali na watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika,Kamanda Kidavashari amewataka wanakatavi kufanya shughuli halali za kujipatia kipato na kutoendelea na vitendo vilivyo kinyume na sheria.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA