WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KATAVI WATAKIWA KUEPUKA MAZINGIRA YA UKATIRI


Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANAFUNZI wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Katavi wametakiwa  kuepuka mazingira yanayopelekea  vitendo ya ukatili na unyanyasaji na  kuzingatia masomo.

Wito huo umetolewa na  Mkuu wa  Kitengo cha dawati la jinsia na  watoto katika Jeshi la Polisi Mkoani Katavi  SP Zabroni  Ibeganisa katika Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Vitendo vya ukatili na unyanyasji wa kijinsia iliyofanyika Shule ya Msingi Kawanzige Manispaa ya Mpanda.
Wanafunzi wa Shule ya ,Msingi Kawanzige
 
Aidha SP Ibeganisa amewataka wanafunzi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa walimu, viongozi wa serikali na dawati la jinsia na watoto kituo cha polisi.
Kauli mbiu ya Kampeni hii mwaka huu ni  Funguka chukua hatua linda mtoto apate elimu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA