MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA POLISI


Na.Mwandishi wetu-Mwanza.
Mahakama kuu kanda ya mwanza imetupilia pingamizi la  polisi kuzuia  waombolezaji kufanya ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa geita Afonce Mawazo aliyeuwawa nov.14 mwakahuu kwa kukatwa mapanga.

Uamuzi huo umefikiwa leo majira ya saa tano asubuhi baada ya Jaji Lameki mlacha kusikiliza kesi ya madai iliyo funguliwa na chadema dhidi ya polisi kuwanyima kibali na kupiga marufuku mkusanyiko wa kuugama mwili wa Marehemu mawazo jijijni Mwanza.

Akizungumza na wananchi baada ya mahakama kutoa uaumzi huo Mwanasheria wa chadema John Mallya amesema kuwa mahakama chini ya Jaji Mlacha imefutilia mbali katazo la polisi kutoaga mwili huo kwasababu ya kipindupindu na usalama kuwa hoja hizo hazina mashiko na kilichobaki ni kupeleka mahakamani nyarajka za kuomba ruhusa ya kuuga mwili huo.
Aidha Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa baada ya masaa mawili nyaraka hizo zitakuwa tayari na kupelekwa mahakamani tayari kwa maamzi ya mahakama.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA