UONGOZI HOSPITALI YA WILAYA MPANDA WALALAMIKIWA KWA KUTOA HUDUMA DUNI KWA WAGONJWA


Na.Issack Gerald-MPANDA
BAADHI ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda wameulalamikia uongozi wa hospital ya wilaya ya Mpanda kwa kutoa huduma isiyoridhisha.

Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA wamesema   huduma inayotolewa hospitalini hapo inacheleweshwa kumfikia mgonjwa.
Aidha  wameiomba serikali kuweka mikakati ya upatikanaji wa damu salama ili kuokoa  maisha ya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya  Wilaya ya Mpanda Dr.Naibu Mkongwa amesema tatizo la ukosekanaji wa damu salama linatokana na wananchi kutokuwa na mwamko wa utoaji damu ili kupungunza ukosefu wa damu.
Wakati huo huo ameiomba serikali kuleta vifaa vya kutosha katika hospital hiyo kwani hospitali hiyo inakabiliwa na  uhaba mkubwa wa vifaa kama vile mipira na dawa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA