WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WALIA NA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA


Na.Issack Gerald-MPANDA
Wakazi wa kata ya Makanyagio katika Manispaa ya  Mpanda Mkoani katavi wameiomba mamlaka ya maji safi na salama Manispaa ya Mpanda kutafuta ufumbuzi wa kuondoa kero ya kukosekana kwa maji safi na salama kwa wananchi hao.

Wakazi hao wametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA na  kusema imekuwa na changamoto ya ukosefu wa maji kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa kero kwa wananchi.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mamla ya maji safi na salama manispaa ya mpanda Injinia Zachari Nyanda amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa mamlaka inafanya jitihada za kubadilisha mabomba chakavu katika maeneo yasiyo na maji.
Licha ya kuwa maeneo Maeneo mengi hayana maji safi na salama katika Manispaa ya Mpanda mitaa ya Kachoma, Majengo A, Majengo B na  madini ni miongoni mwa mitaa iliyoathiriwa zaidi  na ukosefu wa maji.  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA