TUNDU LISSU NAYE AMLILIA MZEE KINGUNGE

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.
Akizungumza leo Februari 2, 2018  ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.”
Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa.
Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane,Oktoba 4,2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.
Tundu Lissu ambaye ni Rais  wa chama cha wanasheria nchini TLS anapatiwa matibabu nchini ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka uliopita.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA