RAIS MAGUFULI AMSAIDIA MLEMAVU BAJAJI

Rais waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw.Yusuf Abdulrahaman Ndemanga.

Bw.Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw.Ngusa Samike,Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Februari 02.
Mhe.Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti,2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na Mhe.Rais Magufuli,Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj ili imsadie kupata kipato.
Akikabidhi msaada huo Bw.Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri na kujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.
Kwa upande wake Bw.Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi.Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA