RAIS MAGUFULI KUWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwa mjibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa kamisheni hizo atazitunuku katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Tukio hilo linatarajia kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari hapa nchini kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA