RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 10:30 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam 22 Desemba 22 mwaka jana.
Mhe.Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali.
Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kufuatia msiba huu,Mhe.Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote,wanachama wa CCM,ndugu,jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu,na amewaombea kuwa na moyo wa subira,uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru mahali pema peponi,Amina.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA