MAGUFULI ATEUA MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali.
Rais wa Tanzania John MagufuliHaki miliki ya pichaREUTERS

Image captionRais wa Tanzania John Magufuli

Kabla ya uteuzi huo Dokta Kilangi,alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino,kituo cha Arusha na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.
Wakati huohuo,Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe,Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.
Kufuatia uteuzi huo,Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.
Uteuzi huo pia umeanza jana Februari mosi.
Jana Rais Dkt.John Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu),na ndiyo maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto kubwa Majaji.

Hata hivyo rais kupitia kilele cha jana cha maadhimisho ya wiki ya sheria Tanzania aliwatuhumu Waziri wa Katiba na Sheria,Prof.Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali,George Masaju na kudai kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo ya msingi.
Kwa mjibu wa taarifa hiyo ambayo imetolewa na katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa kesho Februari 3,2018

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA