SERIKALI KUTOA KAULI YA MAAMUZI KUHUSU VIJIJI VINAVYODAIWA KUWA SEHEMU YA HIFADHI.



Na.Issack Gerald
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kutoa maamuzi baada ya kubaini vijiji vyote nchini vinavyodaiwa kuwa vipo katika maeneo ya hifadhi hapa nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mh.John Peter Kadutu Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu Mkoani Tabora,aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu migogoro baina ya hifadhi na wananchi ambapo baadhi wananchi wanazuiliwa na kufukuzwa licha ya baadhi ya vijiji kusajiliwa na serikali.
Aidha Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwaacha wataalumu wa ardhi wanaobainisha mipaka kati ya hifadhi na vijiji wafanye kazi yao ya kuweka alama kama kawaida.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hivi karibuni alitoa agizo kwa wizara ya Maliasili na utalii kupitia na kuweka mipaka na alama maeneo yote yenye migogoro ya ardhi na wanatakiwa wawe wamekamilisha zoezi hilo mpaka kufikia Desemba 30 mwaka huu ili serikali ichukue maamuzi.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye migogoro ya ardhi baina ya maeneo ya hifadhi na makazi ya watu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA